Wednesday, April 23, 2014

AJALI MBAYA YA MAGARI MANNE YATOKEA MKOANI IRINGA..SHUHUDIA HAPA

Taxi ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika eneo la tukio..
Daladala aina ya Coster yenye namba za usajiri T.960 AQY inayofanya safari zake za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu Tipa, lenye namba SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi.

BASI aina ya Coster linalofanya ruti zake Kibwabwa Manispaa ya Iringa likiwa eneo la tukio, baada ya kugongana na Roli Tipper na kusababisha ajali iliyojeruhi zaidi ya watu 30. ZAIDI ya abiria 38 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne mjini Iringa, baada ya Bus dogo la abiria aina ya Coster kufeli breki na kuyagonga magari matatu, ajali ambayo imetokea majira ya saa saba mchana wa siku ya jana. Tukio hilo limetokea katika mlima wa Ipogolo, eneo maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi", ambapo ajali hiyo imesababisha majeruhi 38 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Iringa, huku chanzo cha ajali hiyo kikisemekana kuwa na kuferi breki kwa Bus hilo la abiria,lenye namba T. 960 AQY na kuyavaa magari matatu, gari kubwa aina ya Tipper Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa, Tax pamoja na Hiace. Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio hilo , Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa Dr. Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na waliolazwa ni 8 huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa majeruhi wengi wameumia zaidi kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi nyumba kwao kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.

MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI IVUMWE, MBEYA YALIVYOUNGUA MOTO..!

 Mwenyekiti wa Bodi wa Kwanza Dr Victory Kanama akiongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM Ndugu Fatma Asenga pamoja na mmoja wa walimu wa shule  hiyo kuangalia namna jnaga hilo la moto lilivyo teketeza mabweni katikia shule hiyo ya Ivumwe yenye mchepuo wa  Wavulana na Wasichana.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Fatma Asenga akizungumza juu ya mipango ya dharula itakayo fanywa ili kuokoa janga hilo.
Na Emanuel Madafa,Mbeya
 Bweni Moja la Wavulana lenye vyumba zaidi ya Sita katika shule ya Sekondari ya Ivumwe inayomilikwa na Chama Cha Mapinduzi limeteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea leo April 23 majira ya saa3 asubuhi jijini Mbeya wakati wanafunzi hao wakiwa madarsani kuendelea na masomo yao kama kawaida.

Akizungumza katika eneo la Tukio hilo Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Daktari Victory Kanama amesema kuwa moto huo umeanza majira ya saa3 asubuhi wakati teyari wanafunzi wakiwa madarasani.

Amesema taarifa za kuungua kwa moto huo zilitolewa na mmoja wa wananchi waliokuwa wakipita pembezoni mwa Mambweni hayo ambapo katika maelezo yake alieleza kuwa ameona moshi mkubwa ukitokea ndani ya mabweni hayo. 

Amesema mara baada ya kupata habari hizo walitoa taarifa kwa kikosi cha zimamoto ambacho kilifika mara moja na kuanza juhudi za kuuzima moto huo. 

Amesema pamoja na kikosi hicho cha zimamoto kufika shuleni hapo mapema na kuzima moto huo lakini teyari moto huo ulikwisha teketeza asilimian kuwabwa ya mali zilizomo katika mabwani hayo.

Amesema kwa kiwango kikubwa vitu vingi vimeteketea kwa moto huo hususani vitanda na magodoro ambayo ndiyo yaliyoungua vibaya pamoja na vitu vingine vya wanafunzi hao. 

Aidha kwa mujibu wa Dakta Kanama hakuna mwanafunzi yoyote aliye poteza maisha kutokana tukio hilo licha ya mmoja wa wanafunzi kujeruhiwa mkononi na kitu kinacho dhaniwa kuwa ni kioo katika harakati za kuokoa vitu ambapo teyari amekwisha fikishwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu. 

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Fatma Asenga amesema mabweni hayo yalichukua jumla ya wanafunzi 160 ambao ni wavulana huku chanzo cha moto huo kikiwa bado bado hakijajulikana. 

Amesema kwa sasa juhudi zinazofanyika na Chama kwa kushirikiana na uongozi wa shule hiyo ili kuangalia uwezekano wa haraka wa kuwahifadhi wanafunzi hao.  Amesema litatengwa darasa moja kwa muda ambalo litatumika kama bweni wakati wakiendela kufanya utaratibu mwingine.

STYLE YA UCHEZAJI YA CHELSEA FC YAWAKERA ATLETICO MADRID...SOMA ZAIDI HAPA..


BAADA ya suluhu pacha ya bila kufungana ( 0-0) na Chelsea, nahodha wa Atletico Madrid, Gabi amekerwa na mbinu ya `kupaki basi` waliyotumia wapinzani wao katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali, ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Atletico wanaosifiwa kujilinda katika ligi ya Hispania, La Liga wamekutana na Chelsea ambayo ina uwezo mkubwa wa `Kupaki basi` kwenye ligi ya England. Katika nusu fainali hii ambayo haitasahaulika kwa Atletico, vinara hao wa La Liga walimiliki mpira kwa asilima 62 na kupiga mashuti 26 golini, wakati Chelsea walipiga mashuti matano tu. 

Matokoe ya leo yanaonekana kuwa mazuri kuelekea mechi ya marudiano darajani, ambapo washambiliaji wawili wa Chelsea Eden Hazard na Samuel Eto`o watarejea uwanjani. 

Gabi amekiri kuwa matokeo ya leo yamewaacha katika hatari kubwa. 

“Hatujaridhika, lakini mechi bado. Atletico walihitaji kushinda kutoka mwanzo wa mchezo hadi mwisho”. 

“ Tulijua Chelsea wasingekubali kufungwa kirahisi na mwisho wa siku tumetoka kapa”. Gabi amewaambia waandishi wa habari.

Atletico hawajafungwa katika michuano ya kimataifa mwaka huu, lakini matokeo ya leo yamewafanya washindwe kupata ushindi kwa mara ya kwanza katika michuano ya ulaya msimu huu wa 2013/2014. 

Katika mechi ya leo, Chelsea wamepatwa na majanga baada ya nahodha wake, John Terry na mlinda mlango namba moja, Petr Cech kupata majeruhi. 

DUH..LADY JAY DEE NDANI YA KASHFA NZITO...MAJIRANI WAMCHANA LIVE...SOMA ZAIDI HAPA...

MAJIRANI wanaoishi karibu na mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Judith Wambura ‘Jide’ wamelalamika kwamba mwanamuziki huyo ameiweka nyumba yake katika mazingira ya uchafu yanayohatarisha maisha yao.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Judith Wambura ‘Jide’.

Wakizungumza na Amani, majirani hao wanaoishi Kimara-Temboni jijini Dar, walisema mwanadada huyo ameacha vichaka vikubwa vinavyoizunguka nyumba yake hali ambayo ni hatari kwani nyoka wanaweza kufanya makazi hivyo kusababisha maafa kwa watoto na watu wazima. 

“Yaani huyu mwanamuziki Jaydee ametuachia kichaka, yeye na mumewe hawataki kufanya usafi kuizunguka nyumba yao hali ambayo inatupa wasiwasi sisi majirani, tuna watoto wanaweza kung’atwa na nyoka kwani nyoka hupenda kuzaliana kwenye vichaka kama hivi,”alisema jirani mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

Waliendelea kusema kuwa, Jide hana hausigeli wala ndugu yeyote anayeishi naye, inawezekana ndiyo maana anashindwa kufanya usafi kuzunguka nyumba yake.
“Lady Jaydee anaishi na mumewe (Gardner) tu labda ndiyo sababu ya kushindwa kutunza mazingira, majani yameota mpaka kero. Tumeshapeleka malalamiko yetu serikali ya mtaa lakini hajaitwa kuambiwa, tunashangaa,” alisema jirani huyo.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Jide na mumewe Gardner ambapo mume huyo ndiye aliyepatikana na kusomewa madai hayo. Baada ya kusikiliza mpaka mwisho, Gardner alijibu:

“Kama wamesema hivyo mimi sina la kujibu (no comment)”.
Juzi, mapaparazi walifika kwenye ofisi ya serikali ya mtaa lakini ilikuwa imefungwa.

SHOCKED: UDHAIFU WA BUNGE LA KATIBA, RAIS JK AOMBWA KULIVUNJA HARAKA IWEZEKANAVYO!

BAADA ya kutokea kwa sintofahamu ndani ya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma kwa wabunge wanaounda umoja wa Ukawa kutoka nje, wengi wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kukivunja chombo hicho.




Rais Jakaya Kikwete akihutubia bungeni Dodoma.


Ukawa ndani ya Bunge wakitoka nje.
“Wote tunajua kwamba kinachotafutwa pale ni katiba ya wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini ni jambo la ajabu kuona wajumbe wanafika pale na kutanguliza misimamo yao na vyama vyao utafikiri ndicho walichotumwa na wananchi, mimi nafikiri JK angelivunjilia mbali bunge hili,” alisema.
Mwanamtwa Palango wa Kurasini, alimlaumu Rais Kikwete kwa kuwajumuisha wabunge kwenye bunge hilo maalum, kwani wao ndiyo chanzo cha kukwamisha mambo mengi ya msingi kupata katiba mpya.

“Hakukuwa na sababu ya kuwajumuisha wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
tumeshawaona hawa ni watu wa malumbano tokea mwanzo, kuwaleta huku ni kuvuruga mambo tu, hapa ilibidi Rais ateue mwenyewe wajumbe wasio wanasiasa. 

INAYOFANANA

QWWWWWWWWWWWWWWW

Popular Posts