Sunday, April 27, 2014

MAJANGA CHADEMA...VIONGOZI WAKE WILAYANI MUFINDI WATIMKIA CCM..!


FAHAMU UGONJWA UNAOWASUMBUA MASTAA WA KIKE BONGO!

Unaweza kuamini ukiambiwa kuwa, umaarufu hapa Bongo unakuja na rangi yake ya kipekee, hata kwa watu wanaochipukia na kutamani kuwa maarufu siku moja, wanaamini kuwa, ili kufanikiwa ni lazima kwanza uwe na rangi nyeupe ya ngozi yako, huwezi kushangaa kwa hili sababu hata Lupita Nyong’o pamoja na kufanikiwa kuwa mwanamke mwenye mvuto mwaka 2014, naye alikuwa anaamini hilo alivyokuwa mdogo.

Saturday, April 26, 2014

AJIRA: TAZAMA NAFASI MPYA ZA KAZI KUTOKA SHIRIKA LA UMEME (TANESCO)


The Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) is focusing on increasing the outreach and service quality of its Energy products for Tanzanian people. Next to its current passion as a leading provider of electricity is to be more efficient and a customer focused utility for Tanzania and beyond.


HABARI PICHA: RAIS KIKWETE ATUNUKU NISHANI NA TUZO ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO

Mama Maria Nyerere akipokea nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano(Order) kwa niaba ya Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

UJUMBE MZITO NA MAALUMU KWA WAPENDA MICHEPUKO‏

Unapenda kuchepuka? Hatukukatazi, lakini tunakupa tahadhari, mchepuko unakuathiri wewe na taifa zima kuanzia sekunde unayoanza, kwa sababu itakupa ugonjwa, utaupeleka nyumbani,

utamwambukiza mwenzako, mtaugua na kufa, mtaiacha yatima familia yenu, mtazalisha watoto wa mitaani, watageuka majambazi na kufanya uhalifu mitaani.

PICHAZ..TAZAMA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO ZAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.


TANZANIA YETs HAVE DONE WELL IN MABWEPANDE -DAR ES SALAAM IN 22th.March 2014.

.

Tuesday, 8 April 2014

TANZANIA YETs HAVE DONE WELL IN MABWEPANDE -DAR ES SALAAM IN 22th.March 2014.

Friday, April 25, 2014

HABARI PICHA: ETI WA MIKOANI MTUACHIE DAR YETU...!

Nafikiri wakati umefika sasa kwa Serikali ianze kuzuia watu kutoka Mikoani kuja Dar, tumetosha sasa! ikiwezekana Waruhusiwe wale tu ambao wamepata kazi au walioitwa kwenye usahili...

AFRIKA YANGARA..MKENYA LUPITA NYONG'O NDIYE MWANAMKE MREMBO ZAIDI DUNIANI..!!!


Lupita Nyong'o mwanamke mrembo zaidi duniani mwaka 2014.
Jarida la People limemtangaza Mkenya Lupita Nyong’o kama mwanamuke mrembo zaidi duniani mwaka 2014.
Lupita ambaye alishinda tuzo ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu '12 years a slave,' yuko kwenye ukurasa wa juu zaidi wa makala ya wiki hii ya jarida hilo.

TABIA CHAFU BONGO MOVIE HASA WASANII WA KIKE..STEVE NYERERE AFUNGUKA, DAWA YAO INAKUJA...!

MWENYEKITI wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa kuna baadhi ya wasanii feki wana tabia chafu zinazoichafua taasisi hiyo, jambo ambalo hawezi kukubaliana nalo.
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akisisitiza jambo.

Akipiga stori na paparazi wetu, kiongozi huyo alisema anashangazwa na wasanii hao wengi wao wakiwa wa kike ambao skendo kwao siyo ishu na wamekuwa wakijitambulisha kama wasanii wa Bongo Muvi.

MASKINI MTITU WA BONGO MOVIE...

MSANII wa filamu za Kibongo, William Mtitu ameelza kuwa, anakesha na kuomba ili Mungu amuwezeshe kumponya baba yake mzazi, Mzee John Mtitu ambaye yuko hoi hospitali kutokana na kuugua kwa muda mrefu.
Mzee John Mtitu akiwa hospitali.

Akizungumza kwa huzuni Mtitu alisema ni muda mrefu umepita tangu baba yake aanze kuugua na  kulazwa Taasisi ya Mifupa Moi akisumbuliwa na uvimbe kichwani hali iliyomsababishia afanyiwe upasuaji.

Msanii wa filamu za Kibongo, William Mtitu.

“Yaani nimehangaika sana na baba yangu, nimemaliza fedha nyingi yaani namuombea tu kwa Mungu amponye maana alifanyiwa upasuaji wa kichwa ni siku tano sasa hajazinduka,” alisema Mtitu.

SHTUKA: FAHAMU ZAIDI KUHUSU UTI "YUTIAI"..UGONJWA UNAOWASUMBUA WADADA WENGI HIVI SASA!

 Tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo kitaalamu linaitwa ‘Urinary Track Infections’ au kwa kifupi ‘UTI’ au imezoeleka kama Yutiai.


Watu wengi wanafahamu Yutiai lakini kila mmoja anaielezea kivyake. Ilimradi tu kuna mabadiliko katika njia ya mkojo au ukeni basi mtu anajua ni Yutiai.
Viungo vinavyohusisha mfumo wa mkojo ni figo, mirija ya kusafirisha mkojo toka katika figo hadi kwenye kibofu chenyewe na njia ya kutolea mkojo nje, Yutiai huathiri sehemu hizi tu.  Endapo mwanamke atatokwa na uchafu ukeni hiyo siyo Yutiai.
Muwasho sehemu za siri pia siyo Yutiai. 

Jinsi tatizo linavyotokea
Maambukizi katika njia ya mkojo huanzia kwenye njia ya kutolea mkojo nje kwa mwanaume na mwanamke. Maambukizi haya yana tabia ya kupanda hadi ndani ya kibofu na kuendelea kwenye ‘Ureter’ hadi kwenye figo.
 

Maambukizi yapo aina nyingi, inaweza kuwa maambukizi ya magonjwa ya ngono au uhamisho wa bakteria wa ukeni na wale wa haja kubwa kwenda kwenye njia ya mkojo. 

Uhamisho unatokana pale mwanamke anapojisafisha ukeni au katika njia ya haja kubwa na kusukumia kwa mbele. Kwa kila binadamu, sehemu ya haja kubwa ina bakteria wake ambao hawana madhara huko lakini wakiingia katika njia ya mkojo wanaleta madhara. 

Wapo bakteria wengine ukeni ambao huko hawana madhara ila wakiingia katika njia ya mkojo wanaleta shida. 

Maambukizi pia huweza kusababishwa na uhamisho wa bakteria kutoka sehemu nyingine  kwenda katika njia ya mkojo. Mfano, kujisafisha sehemu za siri kwa kutumia maji yasiyo safi, kutumia chombo kisicho safi au unapojisaidia yale majimaji yanayokurukia sehemu za siri. 

Nani anaweza kupata Yutiai?
Watu wote wanaume na wanawake wapo hatarini kupata ugonjwa huu. Wanaoathirika zaidi ni wanawake, watoto na wazee.


Wanawake na watoto huathirika zaidi kutokana na sababu za kimaumbile ambapo viungo vya kutolea mkojo na haja kubwa vipo karibu, wazee ni kutokana na kushindwa kujihudumia. 

Wanawake wajawazito pia wapo katika hatari hii kama hawatazingatia usafi wa hali ya juu katika kipindi hiki. 

Wanaume ambao hawajafanyiwa tohara pia wapo katika kundi hili. Wengine ni wanaume wenye tabia ya kulawiti pia husumbuliwa sana na Yutiai na hata kupatwa na tatizo la kuziba kwa njia ya mkojo katika umri wa miaka chini ya 45. Matatizo ya mkojo katika umri zaidi ya miaka 45 hutokana zaidi na hitilafu katika tezi dume. 

Dalili za Yutiai
Mtoto mwenye tatizo hili daima hulialia, hupoteza hamu ya kula na hupatwa na homa za vipindi na hudhoofika.Mwanaume na mwanamke mtu mzima huhisi kuwa mchovu, mkojo kuwa mzito na harufu mbaya na wakati mwingine mkojo huwa na damu. Maumivu chini ya tumbo na huzunguka kiuno na kusambaa miguuni.
 

Huhisi homa au baridi hasa vipindi vya jioni, maumivu husambaa hadi upande wa juu ubavu wa kulia na kushoto, ukikojoa utahisi mkojo wa moto. 

Uchunguzi
Vipimo mbalimbali hufanyika kuangalia athari zinazotokea kutokana na maambukizi.


Kipimo cha kuotesha mkojo ‘Urine Culture and Sensitivity’ ndiyo mahususi kwa ajili ya Yutiai, kipimo hiki majibu yake huchukua zaidi siku mbili na hutumia vifaa maalum kuchukulia mkojo. Kipimo kitaonyesha aina ya bakteria na anakufa kwa dawa gani.
 

ipimo vingine vitafanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa, mfano kipimo cha Ultrasound, vipimo vya damu na vingine. 

Matibabu na ushauri
Tiba hutolewa baada ya majibu ya vipimo. Ni vema kuwa msafi wa maungo na nguo za ndani pamoja na mazingira ya choo.

Kunywa maji mengi kila wakati, kuwa na mkojo wenye rangi iliyokolea siyo dalili ya kuwa na Yutiai.

Wanawake na watoto wadogo wajisafishe kuelekea kwa nyuma, watoto wachanga wasikae na nepi au pambasi zenye mkojo na kinyesi kwa muda mrefu.
Wahi hospitali kwa uchunguzi wa kina.

HUU NDIO UKWELI: INASIKITISHA SANA..TUJIFUNZE TOKA HAPA KWA RAFIKI YETU MR NICE...

Mwanamuziki Nice Lucas Mkenda 'Mr Nice'.
MMOJA wa wasanii waliopata kutamba sana katika muziki wa kizazi kipya ni Nice Lucas Mkenda , maarufu sana mitaani kama Mr Nice. Huyu, kwa wasiomfahamu ni miongoni mwa nyota wa mwanzo mwanzo kabisa wa Bongo Fleva kupata shoo nyingi, ndani na nje ya nchi miaka ile ya 2000.

Jamaa siyo tu anajua kuimba, lakini zaidi alijua namna ya kulimiliki jukwaa, anaweza sana kucheza hasa ile staili ya kukata viuno.Kutokana na uwezo wake huo, ndipo alipoamua kujiita Mfalme wa Takeu, mtindo wake binafsi na staili ya muziki wake alioubuni na kuupatia sana. 

Kama kuna mtu unaweza kumlinganisha na Nice jukwaani, labda anaweza kuwa H. Baba, mkongwe mwingine ambaye pia alikuwa anapiga dizaini kama hiyo. Kazi kubwa na nzuri aliyoifanya ndiyo ilimfanya akimbiliwe sana na mapromota, akialikwa kila mahali Afrika Mashariki na Kati.  

Hivyo haikushangaza, wakati flani miaka ile alipowahi kusema kwamba alikuwa anaingiza kiasi cha shilingi milioni 40 kwa wiki!Alikuwa anaingiza pesa na nafikiri pia alijua kuzitumia.

Kudhihirisha hilo, ni msafara mkubwa aliokuwa akiambatana nao katika harakati zake za kula maisha. Ungeweza kumkuta Club Ambiance kwa mfano akiwa amezungukwa na idadi kubwa ya wapambe. 

Hali kama hiyo ungemkuta nayo pia Kwa Macheni, ile baa maarufu sana pale Magomeni jijini Dar es Salaam, Club Billicanas, Maisha Club na sehemu nyingine zote za starehe. 

Ninaamini kabisa miaka kama saba au zaidi kati ya mwaka 2002 hadi 2010, pesa haikuwa tatizo kwa Mr Nice, mkali wa vibao kama Kidali Po, Fagilia, Kikulacho na Rafiki. 

Wapambe wa Mr Nice wakiwa katika starehe hawakuwahi kupungukiwa vitu mezani, iwe vinywaji au chakula, achilia mbali wale wasio na aibu, walioambatana na mademu zao, kwani bili zao zote zililipwa bila matatizo. 

Leo hii tunapozungumza, sijaonana naye muda mrefu kidogo, lakini nina uhakika huyu siyo yule ambaye wakati flani akielekea Rwanda, aliwahi kupokewa na umati mkubwa wa mashabiki alipotua uwanja wa ndege, wakiongozwa na waziri mmoja wa serikali ya Rais Paul Kagame! 

Hivi karibuni nilipata kuona mahojiano kati yake na chombo kimoja cha habari. Alizungumza mambo mengi yanayohusiana na muziki, maisha na harakati nyingine. Kilichonisukuma kusema naye hapa, ni kauli yake kwamba mambo yanayomtokea ni mipango ya Mungu. 

Hapa alimaanisha kuporomoka kwake kimuziki na bila shaka, kuondoka kwa fedha ‘nyingi’ alizowahi kuzimiliki.Kwanza nimpe pole sana Mr Nice, mmoja kati ya marafiki zangu wengi ndani ya ‘game’ kwa mikasa mfululizo iliyomtokea, kwani katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja alipatwa na majanga mawili makubwa.
Kwanza, akiwa viwanja vyake vya nyumbani, Kona Bar, Sinza Africa Sana alipigwa vibaya na washkaji baada ya kumtuhumu kuwa alitaka kutumia ustaa wake kuwapoka demu wao. 

Siku chache baadaye akapata ajali akiwa ndani ya Bajaj na abiria wenzake wawili aliokuwa nao kufariki dunia, lakini Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema akamponya rafiki yetu Mr Nice.
Ni kweli, Mungu ndiye muweza wa kila jambo.
 

Anaweza kukupandisha na kukushusha akitaka. Lakini wakati mwingine lazima tuwe wakweli ndani ya nafsi zetu.Hivi amekuwezesha kupata fedha, wewe ukakosa mipango nazo, zikapotea, unasema ni mipango yake? 

Mimi nadhani wa kulaumiwa hapa ni Mr Nice mwenyewe. Hili ni tatizo la wengi. Huwa tunadhani kwamba vipaji tulivyopewa tunaweza kuwa navyo milele, wakati ukweli ni kwamba hii huwa ni mitaji tu ya kuweza kutusaidia kutambua fursa nyingine za maisha. Unapopata bahati ya kuingiza fedha nyingi, ni vizuri kuwekeza ili kuweza kujimudu siku zijazo.
Leo hii P Diddy anawaongoza wasanii wa muziki wa Hip Hop wanaoingiza fedha nyingi nchini Marekani, si kwa sanaa, bali kwa uwekezaji alioufanya baada ya kupata pesa kupitia fani hiyo.

TITO VILANONA AFARIKI DUNIA...



TITO VILANOVA AMEFARIKI DUNIA 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Former Barcelona manager Tito Vilanova has passed away aged 45 after losing his battle with throat cancer.

The 45-year-old was taken to the emergency room on Thursday for surgery after being admitted last week when his health worsened. Vilanova had been battling cancer of the throat since 2011 and there had been gastric complications recently.

MFAHAMU MBUNGE MDOGO ZAIDI KATIKA BUNGE LA KATIBA..!


Mbunge Teddy Ladislaus Patrick (21), ndiyo mbunge mdogo kulioko wote katika bunge maalum la katiba linaoendela na vikao vyake mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mh. Samuel Sitta akimuapisha Theddy L. Patrick kuwa mbune wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kati.

Mbunge Theddy L. Patrick akiwasikiliza Wajumbe wengine wa bunge hilo, Mh. Betrice Shelukindo (kulia) na Mh. Hamad Rashid.

KUBWA ZAIDI KUTOKA FACEBOOK NA TIGO...!

Mkurugenzi wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa, Bw. Nicola D’Elia akiongea katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bw. Diego Gutierrez (kushoto).
 
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bw. Diego Gutierrez (kushoto) akiwa amekumbatia na Mkurugenzi wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa, Bw. Nicola D’Elia mara baada ya kumaliza uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bw. Diego Gutierrez (kushoto) na Mkurugenzi wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa, Bw. Nicola D’Elia wakionyesha alama ya 'POA' mara baada ya kumaliza uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Watu waliofika katika uzinduzi huo.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Kampuni ya simu ya mkononi TIGO imetangaza kuingia katika ushirikiano na kampuni ya mtandao wa kijamii Facebook ambapo wateja wake wote nchini watapata huduma ya Facebook bure kwa lugha ya Kiingereza na kwa mara ya kwanza, katika lugha ya Kiswahili kupitia simu zao za mkononi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Facebook kupatikana bila malipo kwa mtandao wowote eneo la Afrika mashariki, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez.

Akizungumza katika tafrija ya uzinduzi wa ushirikiano huo jijini Dar es Salaam, Gutierrez alisema: “Ushirikiano huu unamaanisha kwamba wateja wa Tigo kwa mara ya kwanza watakuwa na uwezo wakutumia Facebook kupitia simu zao za mkononi bila kukatwa gharama yeyote katika utumiaji wa data, hivyo kuwawezesha kuungana na watumiaji wapatao milioni 2 wa mtandao huo wa kijamii waliopo nchini Tanzania kati ya watumiaji bilioni 1.2 duniani kote.”

Gutierrez aliongeza: “Hii ni kwa mara ya kwanza mtandao wowote mkubwa wa kijamii umeweza kupatikanika kwa Kiswahili, lugha ya taifa inayotumika na Watanzania na wingi wa watu walio katika kanda ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika. ”

“Facebook imekuwa chachu kubwa ya utumiaji wa data kwa mitando ya simu. Kwa ushirikiano huu wa kipekee, Tigo imepewa kipaumbele kuliko mitandao mingine katika kuwaletea wateja wengi ladha mpya ya utumiaji waintaneti na mitandao ya kijamii kupitia lugha ya Kiswahili. Hii ndio maana halisi ya maisha ya kidigitali, pia inatimiza malengo yetu ya kuwashawishi wateja wengi zaidi wa Tigo kutumia data katika matumizi yao ya mawasiliano ya kila siku.”

Mkakati huu wa ushirikiano ni muendelezo wa mpango wa Facebook unaoitwa Internet.org uliozinduliwa na muasisi wa kampuni hiyo, Mark Zuckerberg.

Gutierrez alisema, “Huduma hii mpya itafungua milango mipya kwa Watanzania na watumiaji wengine wa Kiswahili kupata fursa za kibiashara, kielimu, na nyinginezo za kijamii na kiuchumi duniani kote.”

Ukiondoa nchi tano wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi, Kiswahili pia kina zungumzwa katika maeneo ya Malawi, Somalia, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Msumbiji.

Kwa uzinduzi huu, Tanzania taifa linayojulikana kama chimbulo la lugha ya Kiswahili, inayofahari ya kuwa nchi ya kwanza katika ukanda huu kutangaza lugha hii kimataifa, mafanikio ambayo hatuna budi yanatokana na ushirikiano kati yaTigo, kampuni mama ya Millicom na Facebook.

Hii ni mara ya pili kwa kampuni ya Facebook na Millicom kushirikiana katika kuzindua huduma ya Facebook kupitia simu bure ambapo Tigo nchini Paraguay walizindua huduma hii kwa mara ya kwanza Desemba 2013 katika lugha ya kiguarani inayotumika nchini humo. Mkurugenzi wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa Nicola D’Elia alisema, “Tunayo furaha kushirikiana na Tigo kwa mara nyingine tena kwa kuwapatia Watanzania wengi zaidi uwezo wa kuwasiliana kupitia utumiaji bure wa data katika app ya Facebook na tovuti ya simu, na sasa katika lugha ya Kiswahili.”

PICHAZ..MATUKIO YA LEO DODOMA WAKATI BUNGE LINAHAIRISHWA..!

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Christopher Ole Sendeka akikanusha taarifa potofu iliyotolewa leo Bunge mjini Dodoma na mjumbe mwenzie wakati wa mjadala wa kurekebisha kanuni za Bunge hilo.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akiongoza mjadala wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya leo mjini Dodoma kabla ya Bunge hilo halihairishwa hadi Agosti mwaka huu.Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ezekeil Oluoch akichangia marekebisho ya Kanuni za Bunge leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa kwa Bunge hilo.Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Asha Bakari Makame akichangia marekebisho ya Kanuni za Bunge leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa kwa Bunge hilo.Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Andrew Chenge akichangia marekebisho ya Kanuni za Bunge leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa kwa Bunge hilo.Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akiwasili kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kuongoza mjadala wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya leo mjini Dodoma kabla ya Bunge hilo halihairishwa hadi Agosti mwaka huu.Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Suleman Jaffo akichangia marekebisho ya Kanuni za Bunge leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa kwa Bunge hilo.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba Mizengo Pinda (kushoto) na Mjumbe wa Bunge hilo Godfrey Zambi wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa kwa Bunge hilo.Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Evod Mmanda akiwasilisha marekebisho ya Kanuni za Bunge leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa kwa Bunge hilo. Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mohamed Seif Khatib(kulia) na Mohamed Aboud Mohamed (kushoto) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa mkutano hadi Agosti mwaka huu. 
Picha na Bunge Maalum la Katiba

Wednesday, April 23, 2014

KAANZA TENA MADUDU..LULU KWELI SIKIO LA KUFA...

Elizabeth Michael ‘Lulu’.
KWAKO Elizabeth Michael ‘Lulu’. Leo nimeona nikukumbuke kupitia barua! Natambua uwezo wako mkubwa katika kazi, juhudi zako binafsi ndiyo zimekufikisha hapo ulipo, mataifa mbalimbali sasa wanatambua kuwa kuna mtu anaitwa Lulu, yupo Bongo, muigizaji!.

Sitaki kukurudisha sana nyuma lakini najua unajua kuwa ni jinsi gani kipindi cha nyuma ulikuwa ukipamba vyombo vya habari kwa skendo chafu. Ulipoteza dira ya kimaisha, watu wengi waliokuwa wakikufuatilia kazi zako walianza kukutupa.

Walikupotezea kwa sababu ya matukio ya ulevi, mavazi ya nusu utupu na matukio mengi ya ajabuajabu yaliyofanana na hayo. Sina nia mbaya kukumbusha lakini waswahili wanasema binadamu anajifunza kutokana na makosa. Maishani mwako umekutana na mazito yasiyofanana na umri wako.
Kwenye ulimwengu wa mahaba, ilikuwepo minong’ono mingi juu ya watu wanaotajwa kushiriki mapenzi na wewe, walitajwa vigogo, mastaa na hata wasio mastaa. Sitaki kusema ni kweli au la lakini lisemwalo kama halipo, ujue laja.
Siri ilifichuka kupitia kifo cha yule unayedai alikuwa mwandani wako, marehemu Steven Kanumba.
Mazingira ya kifo chake, umri mdogo uliokuwa nao ilikuwa ni fundisho kubwa maishani mwako. Ulipambana na msalaba wa gereza, ukapambana na mlolongo wa kesi mahakamani hadi pale ulipofanikiwa kutoka kwa dhamana, Januari mwaka jana.

Baada ya kutoka mahabusu, kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja sasa ulikuwa kimya, ulionekana kubadilika kitabia. Yale uliyokuwa ukiyafanya awali, uliyaweka pembeni na zaidi kusimamia mustakabali mzima wa maisha yako, ulikuwa mwema sana aisee!.
Kinachonisikitisha ni kuanza kusikia tena matukio ya ajabu, unaonekana kubadilika. Nimefuatilia tabia zako, naona umeanza kubadilika, umesahau eeeh! Mavazi yako kwa miezi michache iliyopita, nimegundua yanaanza kuchepuka! Mfano mzuri ni kigauni ulichokivaa mwishoni mwa wiki iliyopita katika sherehe yako ya kuzaliwa.
Hakikustiri maungo yako nyeti, kilionesha sehemu kubwa ya matiti yako.
Kama hiyo haitoshi, kupitia mitandao ya kijamii umeanza kushusha matusi mazito bila sababu za msingi, mtu akikukosoa kidogo, unampa maneno machafu ambayo hayaandikiki gazetini. Kama kioo cha jamii, unapaswa kuvumilia mengi.

Nikiwa kwenye kazi zangu za kila siku, huwa nakuwa wa kwanza kupata fununu za mabadiliko ya kila msanii na namna anavyoishi. Nikuonye tu, kuwa makini na mwenendo wako kwani tayari jamii ilishaanza kujenga imani na wewe. Uliaminika na ndiyo maana ukapata bahati ya kuchukuliwa katika kampuni nzuri ikakusimamia kazi zako hadi sasa.
Kwa kuwa tayari nimeanza kupata malalamiko kutoka katika vyanzo vyangu, nikusihi sana mdogo wangu, usirudi ulipotoka. Jenga heshima mpya na jamii ikuamini kutokana na kazi zako na si skendo za ajabuajabu, kwa leo ni hayo tu!

AJALI MBAYA YA MAGARI MANNE YATOKEA MKOANI IRINGA..SHUHUDIA HAPA

Taxi ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika eneo la tukio..
Daladala aina ya Coster yenye namba za usajiri T.960 AQY inayofanya safari zake za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu Tipa, lenye namba SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi.

BASI aina ya Coster linalofanya ruti zake Kibwabwa Manispaa ya Iringa likiwa eneo la tukio, baada ya kugongana na Roli Tipper na kusababisha ajali iliyojeruhi zaidi ya watu 30. ZAIDI ya abiria 38 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne mjini Iringa, baada ya Bus dogo la abiria aina ya Coster kufeli breki na kuyagonga magari matatu, ajali ambayo imetokea majira ya saa saba mchana wa siku ya jana. Tukio hilo limetokea katika mlima wa Ipogolo, eneo maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi", ambapo ajali hiyo imesababisha majeruhi 38 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Iringa, huku chanzo cha ajali hiyo kikisemekana kuwa na kuferi breki kwa Bus hilo la abiria,lenye namba T. 960 AQY na kuyavaa magari matatu, gari kubwa aina ya Tipper Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa, Tax pamoja na Hiace. Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio hilo , Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa Dr. Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na waliolazwa ni 8 huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa majeruhi wengi wameumia zaidi kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi nyumba kwao kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.

MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI IVUMWE, MBEYA YALIVYOUNGUA MOTO..!

 Mwenyekiti wa Bodi wa Kwanza Dr Victory Kanama akiongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM Ndugu Fatma Asenga pamoja na mmoja wa walimu wa shule  hiyo kuangalia namna jnaga hilo la moto lilivyo teketeza mabweni katikia shule hiyo ya Ivumwe yenye mchepuo wa  Wavulana na Wasichana.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Fatma Asenga akizungumza juu ya mipango ya dharula itakayo fanywa ili kuokoa janga hilo.
Na Emanuel Madafa,Mbeya
 Bweni Moja la Wavulana lenye vyumba zaidi ya Sita katika shule ya Sekondari ya Ivumwe inayomilikwa na Chama Cha Mapinduzi limeteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea leo April 23 majira ya saa3 asubuhi jijini Mbeya wakati wanafunzi hao wakiwa madarsani kuendelea na masomo yao kama kawaida.

Akizungumza katika eneo la Tukio hilo Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Daktari Victory Kanama amesema kuwa moto huo umeanza majira ya saa3 asubuhi wakati teyari wanafunzi wakiwa madarasani.

Amesema taarifa za kuungua kwa moto huo zilitolewa na mmoja wa wananchi waliokuwa wakipita pembezoni mwa Mambweni hayo ambapo katika maelezo yake alieleza kuwa ameona moshi mkubwa ukitokea ndani ya mabweni hayo. 

Amesema mara baada ya kupata habari hizo walitoa taarifa kwa kikosi cha zimamoto ambacho kilifika mara moja na kuanza juhudi za kuuzima moto huo. 

Amesema pamoja na kikosi hicho cha zimamoto kufika shuleni hapo mapema na kuzima moto huo lakini teyari moto huo ulikwisha teketeza asilimian kuwabwa ya mali zilizomo katika mabwani hayo.

Amesema kwa kiwango kikubwa vitu vingi vimeteketea kwa moto huo hususani vitanda na magodoro ambayo ndiyo yaliyoungua vibaya pamoja na vitu vingine vya wanafunzi hao. 

Aidha kwa mujibu wa Dakta Kanama hakuna mwanafunzi yoyote aliye poteza maisha kutokana tukio hilo licha ya mmoja wa wanafunzi kujeruhiwa mkononi na kitu kinacho dhaniwa kuwa ni kioo katika harakati za kuokoa vitu ambapo teyari amekwisha fikishwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu. 

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Fatma Asenga amesema mabweni hayo yalichukua jumla ya wanafunzi 160 ambao ni wavulana huku chanzo cha moto huo kikiwa bado bado hakijajulikana. 

Amesema kwa sasa juhudi zinazofanyika na Chama kwa kushirikiana na uongozi wa shule hiyo ili kuangalia uwezekano wa haraka wa kuwahifadhi wanafunzi hao.  Amesema litatengwa darasa moja kwa muda ambalo litatumika kama bweni wakati wakiendela kufanya utaratibu mwingine.

INAYOFANANA

QWWWWWWWWWWWWWWW

Popular Posts