Friday, April 25, 2014

KUBWA ZAIDI KUTOKA FACEBOOK NA TIGO...!

Mkurugenzi wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa, Bw. Nicola D’Elia akiongea katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bw. Diego Gutierrez (kushoto).
 
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bw. Diego Gutierrez (kushoto) akiwa amekumbatia na Mkurugenzi wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa, Bw. Nicola D’Elia mara baada ya kumaliza uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bw. Diego Gutierrez (kushoto) na Mkurugenzi wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa, Bw. Nicola D’Elia wakionyesha alama ya 'POA' mara baada ya kumaliza uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Watu waliofika katika uzinduzi huo.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Kampuni ya simu ya mkononi TIGO imetangaza kuingia katika ushirikiano na kampuni ya mtandao wa kijamii Facebook ambapo wateja wake wote nchini watapata huduma ya Facebook bure kwa lugha ya Kiingereza na kwa mara ya kwanza, katika lugha ya Kiswahili kupitia simu zao za mkononi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Facebook kupatikana bila malipo kwa mtandao wowote eneo la Afrika mashariki, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez.

Akizungumza katika tafrija ya uzinduzi wa ushirikiano huo jijini Dar es Salaam, Gutierrez alisema: “Ushirikiano huu unamaanisha kwamba wateja wa Tigo kwa mara ya kwanza watakuwa na uwezo wakutumia Facebook kupitia simu zao za mkononi bila kukatwa gharama yeyote katika utumiaji wa data, hivyo kuwawezesha kuungana na watumiaji wapatao milioni 2 wa mtandao huo wa kijamii waliopo nchini Tanzania kati ya watumiaji bilioni 1.2 duniani kote.”

Gutierrez aliongeza: “Hii ni kwa mara ya kwanza mtandao wowote mkubwa wa kijamii umeweza kupatikanika kwa Kiswahili, lugha ya taifa inayotumika na Watanzania na wingi wa watu walio katika kanda ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika. ”

“Facebook imekuwa chachu kubwa ya utumiaji wa data kwa mitando ya simu. Kwa ushirikiano huu wa kipekee, Tigo imepewa kipaumbele kuliko mitandao mingine katika kuwaletea wateja wengi ladha mpya ya utumiaji waintaneti na mitandao ya kijamii kupitia lugha ya Kiswahili. Hii ndio maana halisi ya maisha ya kidigitali, pia inatimiza malengo yetu ya kuwashawishi wateja wengi zaidi wa Tigo kutumia data katika matumizi yao ya mawasiliano ya kila siku.”

Mkakati huu wa ushirikiano ni muendelezo wa mpango wa Facebook unaoitwa Internet.org uliozinduliwa na muasisi wa kampuni hiyo, Mark Zuckerberg.

Gutierrez alisema, “Huduma hii mpya itafungua milango mipya kwa Watanzania na watumiaji wengine wa Kiswahili kupata fursa za kibiashara, kielimu, na nyinginezo za kijamii na kiuchumi duniani kote.”

Ukiondoa nchi tano wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi, Kiswahili pia kina zungumzwa katika maeneo ya Malawi, Somalia, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Msumbiji.

Kwa uzinduzi huu, Tanzania taifa linayojulikana kama chimbulo la lugha ya Kiswahili, inayofahari ya kuwa nchi ya kwanza katika ukanda huu kutangaza lugha hii kimataifa, mafanikio ambayo hatuna budi yanatokana na ushirikiano kati yaTigo, kampuni mama ya Millicom na Facebook.

Hii ni mara ya pili kwa kampuni ya Facebook na Millicom kushirikiana katika kuzindua huduma ya Facebook kupitia simu bure ambapo Tigo nchini Paraguay walizindua huduma hii kwa mara ya kwanza Desemba 2013 katika lugha ya kiguarani inayotumika nchini humo. Mkurugenzi wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa Nicola D’Elia alisema, “Tunayo furaha kushirikiana na Tigo kwa mara nyingine tena kwa kuwapatia Watanzania wengi zaidi uwezo wa kuwasiliana kupitia utumiaji bure wa data katika app ya Facebook na tovuti ya simu, na sasa katika lugha ya Kiswahili.”

PICHAZ..MATUKIO YA LEO DODOMA WAKATI BUNGE LINAHAIRISHWA..!

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Christopher Ole Sendeka akikanusha taarifa potofu iliyotolewa leo Bunge mjini Dodoma na mjumbe mwenzie wakati wa mjadala wa kurekebisha kanuni za Bunge hilo.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akiongoza mjadala wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya leo mjini Dodoma kabla ya Bunge hilo halihairishwa hadi Agosti mwaka huu.Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ezekeil Oluoch akichangia marekebisho ya Kanuni za Bunge leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa kwa Bunge hilo.Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Asha Bakari Makame akichangia marekebisho ya Kanuni za Bunge leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa kwa Bunge hilo.Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Andrew Chenge akichangia marekebisho ya Kanuni za Bunge leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa kwa Bunge hilo.Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akiwasili kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kuongoza mjadala wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya leo mjini Dodoma kabla ya Bunge hilo halihairishwa hadi Agosti mwaka huu.Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Suleman Jaffo akichangia marekebisho ya Kanuni za Bunge leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa kwa Bunge hilo.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba Mizengo Pinda (kushoto) na Mjumbe wa Bunge hilo Godfrey Zambi wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa kwa Bunge hilo.Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Evod Mmanda akiwasilisha marekebisho ya Kanuni za Bunge leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa kwa Bunge hilo. Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mohamed Seif Khatib(kulia) na Mohamed Aboud Mohamed (kushoto) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa mkutano hadi Agosti mwaka huu. 
Picha na Bunge Maalum la Katiba

Wednesday, April 23, 2014

KAANZA TENA MADUDU..LULU KWELI SIKIO LA KUFA...

Elizabeth Michael ‘Lulu’.
KWAKO Elizabeth Michael ‘Lulu’. Leo nimeona nikukumbuke kupitia barua! Natambua uwezo wako mkubwa katika kazi, juhudi zako binafsi ndiyo zimekufikisha hapo ulipo, mataifa mbalimbali sasa wanatambua kuwa kuna mtu anaitwa Lulu, yupo Bongo, muigizaji!.

Sitaki kukurudisha sana nyuma lakini najua unajua kuwa ni jinsi gani kipindi cha nyuma ulikuwa ukipamba vyombo vya habari kwa skendo chafu. Ulipoteza dira ya kimaisha, watu wengi waliokuwa wakikufuatilia kazi zako walianza kukutupa.

Walikupotezea kwa sababu ya matukio ya ulevi, mavazi ya nusu utupu na matukio mengi ya ajabuajabu yaliyofanana na hayo. Sina nia mbaya kukumbusha lakini waswahili wanasema binadamu anajifunza kutokana na makosa. Maishani mwako umekutana na mazito yasiyofanana na umri wako.
Kwenye ulimwengu wa mahaba, ilikuwepo minong’ono mingi juu ya watu wanaotajwa kushiriki mapenzi na wewe, walitajwa vigogo, mastaa na hata wasio mastaa. Sitaki kusema ni kweli au la lakini lisemwalo kama halipo, ujue laja.
Siri ilifichuka kupitia kifo cha yule unayedai alikuwa mwandani wako, marehemu Steven Kanumba.
Mazingira ya kifo chake, umri mdogo uliokuwa nao ilikuwa ni fundisho kubwa maishani mwako. Ulipambana na msalaba wa gereza, ukapambana na mlolongo wa kesi mahakamani hadi pale ulipofanikiwa kutoka kwa dhamana, Januari mwaka jana.

Baada ya kutoka mahabusu, kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja sasa ulikuwa kimya, ulionekana kubadilika kitabia. Yale uliyokuwa ukiyafanya awali, uliyaweka pembeni na zaidi kusimamia mustakabali mzima wa maisha yako, ulikuwa mwema sana aisee!.
Kinachonisikitisha ni kuanza kusikia tena matukio ya ajabu, unaonekana kubadilika. Nimefuatilia tabia zako, naona umeanza kubadilika, umesahau eeeh! Mavazi yako kwa miezi michache iliyopita, nimegundua yanaanza kuchepuka! Mfano mzuri ni kigauni ulichokivaa mwishoni mwa wiki iliyopita katika sherehe yako ya kuzaliwa.
Hakikustiri maungo yako nyeti, kilionesha sehemu kubwa ya matiti yako.
Kama hiyo haitoshi, kupitia mitandao ya kijamii umeanza kushusha matusi mazito bila sababu za msingi, mtu akikukosoa kidogo, unampa maneno machafu ambayo hayaandikiki gazetini. Kama kioo cha jamii, unapaswa kuvumilia mengi.

Nikiwa kwenye kazi zangu za kila siku, huwa nakuwa wa kwanza kupata fununu za mabadiliko ya kila msanii na namna anavyoishi. Nikuonye tu, kuwa makini na mwenendo wako kwani tayari jamii ilishaanza kujenga imani na wewe. Uliaminika na ndiyo maana ukapata bahati ya kuchukuliwa katika kampuni nzuri ikakusimamia kazi zako hadi sasa.
Kwa kuwa tayari nimeanza kupata malalamiko kutoka katika vyanzo vyangu, nikusihi sana mdogo wangu, usirudi ulipotoka. Jenga heshima mpya na jamii ikuamini kutokana na kazi zako na si skendo za ajabuajabu, kwa leo ni hayo tu!

AJALI MBAYA YA MAGARI MANNE YATOKEA MKOANI IRINGA..SHUHUDIA HAPA

Taxi ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika eneo la tukio..
Daladala aina ya Coster yenye namba za usajiri T.960 AQY inayofanya safari zake za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu Tipa, lenye namba SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi.

BASI aina ya Coster linalofanya ruti zake Kibwabwa Manispaa ya Iringa likiwa eneo la tukio, baada ya kugongana na Roli Tipper na kusababisha ajali iliyojeruhi zaidi ya watu 30. ZAIDI ya abiria 38 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne mjini Iringa, baada ya Bus dogo la abiria aina ya Coster kufeli breki na kuyagonga magari matatu, ajali ambayo imetokea majira ya saa saba mchana wa siku ya jana. Tukio hilo limetokea katika mlima wa Ipogolo, eneo maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi", ambapo ajali hiyo imesababisha majeruhi 38 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Iringa, huku chanzo cha ajali hiyo kikisemekana kuwa na kuferi breki kwa Bus hilo la abiria,lenye namba T. 960 AQY na kuyavaa magari matatu, gari kubwa aina ya Tipper Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa, Tax pamoja na Hiace. Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio hilo , Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa Dr. Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na waliolazwa ni 8 huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa majeruhi wengi wameumia zaidi kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi nyumba kwao kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.

MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI IVUMWE, MBEYA YALIVYOUNGUA MOTO..!

 Mwenyekiti wa Bodi wa Kwanza Dr Victory Kanama akiongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM Ndugu Fatma Asenga pamoja na mmoja wa walimu wa shule  hiyo kuangalia namna jnaga hilo la moto lilivyo teketeza mabweni katikia shule hiyo ya Ivumwe yenye mchepuo wa  Wavulana na Wasichana.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Fatma Asenga akizungumza juu ya mipango ya dharula itakayo fanywa ili kuokoa janga hilo.
Na Emanuel Madafa,Mbeya
 Bweni Moja la Wavulana lenye vyumba zaidi ya Sita katika shule ya Sekondari ya Ivumwe inayomilikwa na Chama Cha Mapinduzi limeteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea leo April 23 majira ya saa3 asubuhi jijini Mbeya wakati wanafunzi hao wakiwa madarsani kuendelea na masomo yao kama kawaida.

Akizungumza katika eneo la Tukio hilo Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Daktari Victory Kanama amesema kuwa moto huo umeanza majira ya saa3 asubuhi wakati teyari wanafunzi wakiwa madarasani.

Amesema taarifa za kuungua kwa moto huo zilitolewa na mmoja wa wananchi waliokuwa wakipita pembezoni mwa Mambweni hayo ambapo katika maelezo yake alieleza kuwa ameona moshi mkubwa ukitokea ndani ya mabweni hayo. 

Amesema mara baada ya kupata habari hizo walitoa taarifa kwa kikosi cha zimamoto ambacho kilifika mara moja na kuanza juhudi za kuuzima moto huo. 

Amesema pamoja na kikosi hicho cha zimamoto kufika shuleni hapo mapema na kuzima moto huo lakini teyari moto huo ulikwisha teketeza asilimian kuwabwa ya mali zilizomo katika mabwani hayo.

Amesema kwa kiwango kikubwa vitu vingi vimeteketea kwa moto huo hususani vitanda na magodoro ambayo ndiyo yaliyoungua vibaya pamoja na vitu vingine vya wanafunzi hao. 

Aidha kwa mujibu wa Dakta Kanama hakuna mwanafunzi yoyote aliye poteza maisha kutokana tukio hilo licha ya mmoja wa wanafunzi kujeruhiwa mkononi na kitu kinacho dhaniwa kuwa ni kioo katika harakati za kuokoa vitu ambapo teyari amekwisha fikishwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu. 

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Fatma Asenga amesema mabweni hayo yalichukua jumla ya wanafunzi 160 ambao ni wavulana huku chanzo cha moto huo kikiwa bado bado hakijajulikana. 

Amesema kwa sasa juhudi zinazofanyika na Chama kwa kushirikiana na uongozi wa shule hiyo ili kuangalia uwezekano wa haraka wa kuwahifadhi wanafunzi hao.  Amesema litatengwa darasa moja kwa muda ambalo litatumika kama bweni wakati wakiendela kufanya utaratibu mwingine.

INAYOFANANA

QWWWWWWWWWWWWWWW

Popular Posts