Wednesday, April 23, 2014

STYLE YA UCHEZAJI YA CHELSEA FC YAWAKERA ATLETICO MADRID...SOMA ZAIDI HAPA..


BAADA ya suluhu pacha ya bila kufungana ( 0-0) na Chelsea, nahodha wa Atletico Madrid, Gabi amekerwa na mbinu ya `kupaki basi` waliyotumia wapinzani wao katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali, ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Atletico wanaosifiwa kujilinda katika ligi ya Hispania, La Liga wamekutana na Chelsea ambayo ina uwezo mkubwa wa `Kupaki basi` kwenye ligi ya England. Katika nusu fainali hii ambayo haitasahaulika kwa Atletico, vinara hao wa La Liga walimiliki mpira kwa asilima 62 na kupiga mashuti 26 golini, wakati Chelsea walipiga mashuti matano tu. 

Matokoe ya leo yanaonekana kuwa mazuri kuelekea mechi ya marudiano darajani, ambapo washambiliaji wawili wa Chelsea Eden Hazard na Samuel Eto`o watarejea uwanjani. 

Gabi amekiri kuwa matokeo ya leo yamewaacha katika hatari kubwa. 

“Hatujaridhika, lakini mechi bado. Atletico walihitaji kushinda kutoka mwanzo wa mchezo hadi mwisho”. 

“ Tulijua Chelsea wasingekubali kufungwa kirahisi na mwisho wa siku tumetoka kapa”. Gabi amewaambia waandishi wa habari.

Atletico hawajafungwa katika michuano ya kimataifa mwaka huu, lakini matokeo ya leo yamewafanya washindwe kupata ushindi kwa mara ya kwanza katika michuano ya ulaya msimu huu wa 2013/2014. 

Katika mechi ya leo, Chelsea wamepatwa na majanga baada ya nahodha wake, John Terry na mlinda mlango namba moja, Petr Cech kupata majeruhi. 

DUH..LADY JAY DEE NDANI YA KASHFA NZITO...MAJIRANI WAMCHANA LIVE...SOMA ZAIDI HAPA...

MAJIRANI wanaoishi karibu na mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Judith Wambura ‘Jide’ wamelalamika kwamba mwanamuziki huyo ameiweka nyumba yake katika mazingira ya uchafu yanayohatarisha maisha yao.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Judith Wambura ‘Jide’.

Wakizungumza na Amani, majirani hao wanaoishi Kimara-Temboni jijini Dar, walisema mwanadada huyo ameacha vichaka vikubwa vinavyoizunguka nyumba yake hali ambayo ni hatari kwani nyoka wanaweza kufanya makazi hivyo kusababisha maafa kwa watoto na watu wazima. 

“Yaani huyu mwanamuziki Jaydee ametuachia kichaka, yeye na mumewe hawataki kufanya usafi kuizunguka nyumba yao hali ambayo inatupa wasiwasi sisi majirani, tuna watoto wanaweza kung’atwa na nyoka kwani nyoka hupenda kuzaliana kwenye vichaka kama hivi,”alisema jirani mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

Waliendelea kusema kuwa, Jide hana hausigeli wala ndugu yeyote anayeishi naye, inawezekana ndiyo maana anashindwa kufanya usafi kuzunguka nyumba yake.
“Lady Jaydee anaishi na mumewe (Gardner) tu labda ndiyo sababu ya kushindwa kutunza mazingira, majani yameota mpaka kero. Tumeshapeleka malalamiko yetu serikali ya mtaa lakini hajaitwa kuambiwa, tunashangaa,” alisema jirani huyo.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Jide na mumewe Gardner ambapo mume huyo ndiye aliyepatikana na kusomewa madai hayo. Baada ya kusikiliza mpaka mwisho, Gardner alijibu:

“Kama wamesema hivyo mimi sina la kujibu (no comment)”.
Juzi, mapaparazi walifika kwenye ofisi ya serikali ya mtaa lakini ilikuwa imefungwa.

SHOCKED: UDHAIFU WA BUNGE LA KATIBA, RAIS JK AOMBWA KULIVUNJA HARAKA IWEZEKANAVYO!

BAADA ya kutokea kwa sintofahamu ndani ya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma kwa wabunge wanaounda umoja wa Ukawa kutoka nje, wengi wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kukivunja chombo hicho.




Rais Jakaya Kikwete akihutubia bungeni Dodoma.


Ukawa ndani ya Bunge wakitoka nje.
“Wote tunajua kwamba kinachotafutwa pale ni katiba ya wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini ni jambo la ajabu kuona wajumbe wanafika pale na kutanguliza misimamo yao na vyama vyao utafikiri ndicho walichotumwa na wananchi, mimi nafikiri JK angelivunjilia mbali bunge hili,” alisema.
Mwanamtwa Palango wa Kurasini, alimlaumu Rais Kikwete kwa kuwajumuisha wabunge kwenye bunge hilo maalum, kwani wao ndiyo chanzo cha kukwamisha mambo mengi ya msingi kupata katiba mpya.

“Hakukuwa na sababu ya kuwajumuisha wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
tumeshawaona hawa ni watu wa malumbano tokea mwanzo, kuwaleta huku ni kuvuruga mambo tu, hapa ilibidi Rais ateue mwenyewe wajumbe wasio wanasiasa. 

Friday, March 7, 2014

OOOH..KUHUSUI BINTI WA RAISI MUSEVEN WA UGANDA KUKIRI KUWA NI MSAGAJI...!JIONEE MWENYEWE UKWELI HAPA...

Abril Uno, ni jina lenye maana ya ’1 April’ kwa Kihispania, ambayo ni siku ya wajinga.Ile taarifa iliyoonekana kuchanganya watu na kutokana na kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii hapo jana ya kwamba mtoto wa kike wa Rais wa Uganda alijitangaza kuwa ni msagaji, taarifa hiyo sio ya kweli.
Imeelezwa kwamba habari hiyo ilianzia kwenye mtandao mmoja wa nchini Marekani itwao Abril Uno, ambao uliandika habari hiyo wiki iliyopita siku ya Jumatano.

Kwenye tarifa yake mtandao huo ulitania kwa kuandika kwamba Diana Kamuntu, mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amejitangaza kuwa ni msagaji kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio.

Taarifa hiyo ilisema: “Mimi ni msagaji, ninafanya mapenzi ya jinsia moja. Nimelijua hilo toka nilivyokuwa msichana mdogo,” taarifa ilimnukuu Kamuntu.
Kwenye mtandao wa Abril Uno ulimtaja muendesha kipindi wa redio hiyo James Kasirivu, kuwa ndiye aliyekuwa akifanya mahojiano hayo, na kusema kwamba “alipatwa na mshangao na mpaka aliishiwa na maneno ya kuongea toka kinywani mwake.”

Maelezo hayo yalisambaa kwenye mitandao mingi Duniani, huku wengine kuitoa na wengine kuiacha.

Watu wengi waliguswa na taarifa hiyo huku baadhi yao wakiandika kwenye kurasa zao za Twitter katika hali ya kumuunga mkono Kamuntu:


Abril Uno, ni jina lenye maana ya ’1 April’ kwa Kihispania, ambayo ni siku ya wajinga.

Hivyo akili Kichwani Mwako. 
via-abri uno, PointBlankNews

KIMENUKA..WABUNGE WA KENYA NAO WATAKA SHERIA KALI DHIDI YA MASHOGA NA WASAGAJI...!SOMA ZAIDI HAPA...!

Mwandishi vitabu Binyavanga Wainaina aliyetangaza majuzi kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja
Mbunge Irungu Kang'ata anaongoza juhudi za kundi lililoundwa majuzi la kupinga wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya. Sheria zilizopo zasema ni hatia kwa watu kujiingiza katika tabia za ushoga na adhabu yake ni kifungo cha miaka 14 jela.

Kenya huenda ikawa nchi inayofuata kwenye utata unaohusiana na haki za wapenzi wa jinsia moja, huku wabunge wakipanga kuwasilisha mswada bungeni kushinikiza serikali kufanya juhudi zaidi kutekeleza sheria zilizomo za kupiga marufuku ushoga.

Nao wanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanasema shinikizo limeongezeka tangu nchi jirani ya Uganda kupitisha sheria dhidi ya mashoga mwezi jana.

Irungu Kang'ata, ambaye ni mbunge kwa mara ya kwanza anaongoza juhudi za kundi lililoundwa majuzi la kupinga wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya. Katika kampeni wazi kabisa mbunge huyo ameomba chama tawala kuelezea serikali inachukua hatua gani kutekeleza sheria zilizopo dhidi ya mashoga.

Sheria zilizopo nchini Kenya zinasema ni hatia kwa watu kujiingiza katika tabia za ushoga na adhabu yake ni kifungo cha miaka 14 jela. Hakuna aliyewahi kushtakiwa nchini humo, lakini wanaharakati wanasema kuna kesi takriban 8 mahakamani ambazo hazijaamuliwa.

Kundi hilo linalopinga wapenzi wa jinsia moja liliundwa majuzi wakati rais wa nchi jirani ya Uganda Yoweri Museveni alipotia saini sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja mwezi Februari, licha ya shinikizo kutoka kwa nchi za Magharibi asitie saini.Sasa ushoga huko Uganda ni kosa linaloweza kuadhibiwa kwa kifungo cha maisha jela.

Mbunge Kang'ata anasema anataka kuwasilisha mswada mpya utakaokuwa na adhabu kali zaidi nchini Kenya ikiwa bunge litaamua kuwa sheria zilizopo hivi sasa hazitoshi. Na anawashauri mashoga wajiepushe na matatizo haya kwa 'kufyata midomo'.

Lakini kwa mkurugenzi wa kundi la kitaifa la tume ya haki za mashoga Kenya, Eric Gitari anasema shinikizo hili dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ni njia moja ya kugubika matatizo ya kisiasa yaliyomo na ukiukwaji wa haki za kibinafsi.

Gitari ambaye ni wakili wa kutetea haki za binadamu, anapinga pendekezo kwamba wapenzi wa jinsia moja wakae kimya, akisisitiza kuwa ni wanasiasa wanaolieneza swala hili kwa umma. Kama mwanamume ambaye ni shoga anasema mara nyingi anajihisi kama raia wa daraja la pili Naye mwanaharakati wa kibinafsi Kenne Mwikya, anasema hisia nchini Kenya zinaweka mazingira yafaayo kwa watu kama mbunge Irungu Kang'ata kuamua kuwa wanapaswa kubuni sheria mpya dhidi ya wapenzi wa jinsia moja au kutekeleza sheria zizilizopo.

INAYOFANANA

QWWWWWWWWWWWWWWW

Popular Posts